Isaiah 9:15-17


15 aWazee na watu mashuhuri ndio vichwa,
nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia.

16 bWale wanaowaongoza watu hawa wanawapotosha,
nao wale wanaoongozwa wamepotoka.

17 cKwa hiyo Bwana hatawafurahia vijana,
wala hatawahurumia yatima na wajane,
kwa kuwa kila mmoja wao hamchi Mungu, nao ni waovu,
na kila kinywa kinanena upotovu.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.

Copyright information for SwhKC